Real Madrid imeiangushia Rayo Vallecano kipigo cha mbwa mwizi baada ya kuibugiza bao 10-2 katika mchezo wa La Liga uliochezwa Jumapili kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu.
Gareth Bale akafunga mara nne huku Karim Benzema mara tatu na Cristiano Ronaldo akitupia mpira wavuni mara mbili.
Bao lingine la Real Madrid lilifungwa na Danilo wakati magoli ya Rayo Vallecano, iliyopoteza wachezaji wawili kwa kadi nyekundu yalifungwa na Amaya na Jozabed.
Real Madrid: Navas, Danilo, Pepe, Ramos, Marcelo (Vazquez 62), Kroos, Modric, Rodriguez (Kovavic 65), Ronaldo, Benzema, Bale (Arbeloa 74).
Subs not used: Casilla, Nacho, Casemiro, Isco.
Wafungaji: Danilo 3, Bale 25, 41, 61, 70, Ronaldo 30, 53, Benzema 48, 79, 90
Rayo Vallecano: Yoel, Tito, Ze Castro (Cabellero 80), Amaya, Nacho, Baena, Trashorras, Bangoura (Bebe 63), Jozabed, Pablo Hernandez (Quini 21), Javi Guerra.
Subs not used: Corral, Dorado, Manucho, Embarba.
Wafungaji: Amaya 10, Jozabed 12
Gareth Bale amefunga magoli manne Real Madrid ikiichapa Rayo Vallecano 10-2 kwenye mchezo wa La Liga uliochezwa Jumapili
Bale (kushoto) akifunga bao lake la nne dakika ya 70
Cristiano Ronaldo naye alikuwemo kwenye orodha ya wafungaji
Bale akifanya matokeo yasomeke 4-2
Bale anashangilia
Karim Benzema akiifungia Real Madrid bao la tano
Ronaldo (katikati) akiifungia Real Madrid goli la sita dakika ya 53
Bale (kulia) akimshukuru Ronaldo
Comments
Post a Comment