REAL MADRID YAFANYA MAUAJI, YAPIGA MTU 8-0 …Ronaldo afunga 4 na kuweka rekodi mpya, Paris Saint Germain nayo yashinda
Cristiano Ronaldo              ameweka rekodi mpya hatua ya makundi Champions League wakati              Real Madrid ikiichapa Malmo bao 8-0.
        Ronaldo akafunga              mara nne na kufanikiwa kujikusanyia jumla ya mabao 11 hatua              ya makundi ambayo ni rekodi mpya kwenye michuano hiyo.
        Karim Benzema naye akafunga mara              tatu huku bao lingine la Real Madrid likifungwa na Mateo              Kovacic.
        Hata kabla ya mchezo huo, Real              Madrid ilishajihakikishia nafasi ya kwanza kwenye kundi A,              lakini hiyo haikuwa sababu ya kuacha kuingushia Malmo kipigo              cha mbwa mwizi.
        Katika mchezo            mwingine wa kundi hilo, Paris Saint Germain iliyoshika nafasi            ya pili, ikaichapa Shakhtar Donetsk 2 – 0 kwa magoli ya Lucas            Moura na Zlatan Ibrahimovic.
        Ronaldo                akifunga moja ya mabao yake manne
          Ronaldo                akishangilia bao lake la tatu
            
Comments
Post a Comment