Hali ya klabu ya Real Madrid katika msimu mpya wa ligi kuu ya Uhispania sio nzuri na inazidisha presha kwa kocha Rafa Benitez kila kukicha huku baadhi ya wadau wakianza kushinikiza atimuliwe kazi.
Watu mbalimbali mashuhuri wamekuwa wakizungumzia kile kinachoikumba Madrid katika siku za hivi karibuni, mmoja wao ni mkurugenzi wa soka wa zamani wa Real Madrid, Arrigo Sacchi, ambaye amesema kwamba klabu hiyo imeshindwa kuendelea pale alipoachia Carlo Ancelotti mpaka kwa Rafa Benítez "kiufundi na kimbinu pamoja na kisaikolojia'.
Akizungumza na 'La Gazzetta dello Sport', Sacchi alisema anafikri kwamba "Benítez bado haja connect vizuri na mashabiki na Raisi Florentino Pérez".
Real Madrid ni kikosi kilichojaa mastaa mbalimbali lakini sio timu", alisema Sacchi. "Wana wachezaji wenye uwezo binafsi kuliko walio na mfumo wa kucheza kitimu na kocha analazimika kuendelea kuipanga timu hiyo bila kukosana na utawala wa timu. Kikosi chao ni mkusanyiko wa mastaa, ambao kuna uwezekano wakawa ni bora duniani, lakini hawachezi kitimu."
Comments
Post a Comment