RAFAEL BENITEZ ASEMA HANA TATIZO NA BENZEMA LICHA YA KUFUNGIWA TIMU YA TAIFA



RAFAEL BENITEZ ASEMA HANA TATIZO NA BENZEMA LICHA YA KUFUNGIWA TIMU YA TAIFA
Karim Benzema looks            set to miss out on a place at Euro 2016 with France due to an            ongoing investigation
KOCHA wa Real Madrid Rafael Benitez, amemwelezea staa wake Karim Benzema (pichani juu) kuwa ni mtu safi baada ya nyota huyo kujikuta matatani nchini kwao Ufaransa.

Wiki iliyopita Benzema alisimamishwa kuchezea timu ya taifa ya Ufaransa ili kusubiri matokeo ya uchunguzi kuhusu kashfa ya kuingiza picha ya ngono mtandaoni akiwa na mchezaji mwenzake Mathieu Valbuena.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 27, kwa sasa amefunguliwa mashitaka kutokana na kashfa hiyo ingawa anakana tuhuma hizo.

Licha ya kukumbana na balaa hilo, Benzema anaonekna kutokuwa na matatizo uwanjani baada ya wiki iliyopita kufunga mabao mawili katika ushindi wa 4 - 1 dhidi ya Getafe na katikati ya wiki iliyopita akatupia hat-trick katika ushindi wa mabao 8-0 dhidi ya Malmo katika michuano ya Klabu Bingwa Ulaya.

Benetez anamuunga mkono nyota huyo wa zamani wa timu ya Lyon katika matatizo yanayomkabili.

"Kinachonisononesha mimi kuhusu Karim ni kufungiwa na Ufaransa, ila tunamuunga mkono kwa asilimia mia moja kutokana na kwamba ni mchezaji wetu mzuri na ni mtu safi," alisema Benetez.


Comments