KOCHA mkuu wa timu ya Real Madrid ya Hispania, Rafa            Benitez, ametamba kuwa bado anapenda kusajili mchezaji mmoja            mwenye kasi ya kukimbia ili aweze kupata mabao zaidi.
        Benitez amesema amekuwa akipata wakati mgumu kutokana            na kukosa mtu mwenye mbio za kushitukiza wa kusaidiana na            Cristiano Ronaldo na Karim Benzema.
        "Yapo baadhi ya mambo kwa upande wangu ni magumu, hasa            kipindi cha usajili cha dirisha dogo, nimepanga kusajili            mshambuliaji lakini nina kila sababu ya kujipanga ili kumnasa            nyota ambaye ana msaada mkubwa ndani ya dimba," alisema kocha            huyo.
        Hata hivyo, Benzema alisema kwamba bado anaendelea na            kazi hiyo kwa usiri mkubwa asije akavurugiwa na baadhi ya            makocha wa timu nyingine.
        
Comments
Post a Comment