KOCHA wa Real Madrid, Rafa Benitez amesema ana imani kubwa ya kumnasa mshambuliaji wa Bayern Munich, Robert Lewandowski katika msimu ujao.
Benetez alisema kuwa amekuwa akivutiwa na uwezo mkubwa wa mchezaji huyo kwa namna anavyoweza kuwahadaa mabeki na ubora wake wa kuwachambua magolikipa hata pale anapokuwa na nafasi finyu.
Habari za ndani kutoka Madrid zinadai kuwa timu hiyo tayari imeanza mikakati ya kimya kimya kuhakikisha inamnasa staa huyo wa Poland licha ya kuwepo ushindani kutoka kwa timu kadhaa barani Ulaya.
"Huyu ni mchezaji mzuri, lakini anaweza kuwa mkali zaidi akija hapa Madrid, kazi hiyo imeanza kufanyika kwa mafanikio makubwa," kilisema chanzo kimoja cha Real Madrid.
Comments
Post a Comment