PETR CECH ASEMA UBINGWA WA LIGI KUU HAUKWEPEKI ARSENAL



Petr Cech waves to the            Arsenal fans having secured his 170th Premier League clean            sheet on Monday
WACHEZAJI wa Arsenal wakiongozwa na kipa mkongwe, Petr Cech, wamejitapa kwamba msimu huu watatwaa ubingwa wa Ligi Kuu England.

Jeuri hiyo ya Arsenal imekuja baada ya klabu hiyo kufanikiwa kumaliza nusu ya msimu huku ikiwa kileleni mwa Ligi Kuu.

 "Ukiangalia tangu kuanza kwa msimu huu, tumepoteza michezo minne tu hadi kufikia mwisho wa Disemba, sio kazi rahisi, nadhani tunaweza kuhitimisha vizuri," alisema Petr Cech aliyeweka rekodi mpya England ya kuwa akipa aliyecheza mechi nyingi bila kufungwa (clean sheet).

Cech mwenye miaka 33, ambaye ni kipa aliyeipa mafanikio makubwa Chelsea kabla ya kutupiwa virago mwishoni mwa msimu uliopita, alisema wachezaji watapigania ushindi kila mechi.

Aliongeza kusema kuwa, ikiwa wameweza kuituliza Manchester City, haoni ni kwanini washindwe kuzifunga timu nyingine.

Arsenal haijawahi kutwaa taji la Ligi Kuu tangu msimu wa 2003-04 ilipoandika historia ya kutopoteza mchezo hata mmoja.

Hata hivyo, kocha wa Arsenal amelia kuwakosa wachezaji kadha muhimu wa kikosi chake kutokana na kuwa majeruhi, wakiwemo Jack Wilshere, Francis Coquelin, Danny welbeck, Sant Cazorla na Tomas Rosicky.


Comments