PEP GUARDIOLA ASEMA ANAONDOKA BAYERN MSIMU HUU ...Manchester City, lakini mashabiki wa United na Chelsea kuingia kiwewe
Pep Guardiola atatangaza kuachana na Bayern Munich wiki ijayo huku kocha wa zamani wa Carlo Ancelotti akipewa nafasi kubwa kurithi kiti cha ukocha Allianz Arena.
Inadaiwa Guardiola ambaye mkataba wake unafikia kikomo mwishoni mwa msimu huu, ameamua kutoongeza mkataba mwingine Bayern Munich.
Habari hizo zitapokewa kwa shauku kubwa na vilabu vya Chelsea, Manchester United na Manchester City ambazo zote zinaripotiwa kutoridhika na huduma za makocha wao wa sasa hivi.
Guardiola anatarajiwa kujiunga na Manchester City, lakini mashabiki wa United na Chelsea watahoji: "Kwanini hatajajaribu kumsainisha kwetu?"
Ancelotti amekuwa akihusishwa na kurejea Chelsea lakini kcoha huyo wa zamani wa Real Madrid hana fikra za kufundisha tena Stamford Bridge.
Kocha wa Bayern Munich Pep Guardiola amethibithsa kuwa ataondoka kwenye klabu hiyo
Guardio kuonda Bayern Munich mwishoni mwa msimu
Guardiola aliichukua Bayern Munich baada ya kushinda mataji matatu mwaka 2013 na akafanikiwa kutetea taji la Bundesliga mara mbili mfululizo.
Mhispania huyo amesema atafafanua hatma yake wiki ijayo. "Leo sina jibu," alisema Jumanne usiku baada ya ushindi dhidi ya Darmstadt. Wiki ijayo nitaweka mambo hadharani.
Carlo Ancelotti huenda akamrithi Guardiola
Comments
Post a Comment