Mesut Ozil anahisi kuwa kocha wake wa zamani Jose Mourinho anaweza akaifanya Man United kurudi katika ubora wake tena kama zamani.
Mourinho aalifukuzwa na Chelsea wiki iliyopita baada ya mfululizo wa matokeo mabovu kwa klabu hiyo huku ikidizi kudidimia na kukaribia nafasi za kushuka daraja.
Licha ya kufukuzwa Chelsea kwa mara ya pili, Mourinho amekuwa akihusishwa na vilabu kadhaa vikubwa barani Ulaya, hasa Manchester United ambaye kocha wake wa sasa Louis Van Gaal akiwa kwenye presha kubwa ya kufukuzwa baada ya mfululizo wa matokeo mabaya klabuni hapo.
Ozil, ambaye alikuwa ni moja ya wachezaji muhimu walioipa 'ndoo' Real Madrid enzi za Mourinho, amekiri kuwa ameshtushwa na matatizo yaliyomkumba kocha wake huyo wa zamani lakini akiamini kwamba atapata mafanikio makubwa atakapoenda klabuni nyingine.
"Nimeshangazwa sana na kilichomtokea Jose", alisema wakati akizungumza na The Times.
"Ni kocha mkubwa. Naamini kwamba klabu yoyote atakayoenda kuanzia sasa atafanikiwa kwa mara nyingine tena".
"Najua ni jinsi gani alivyo kocha wa aina yake. Nikocha mkubwa ambaye mara zote amekuwa akitoa sapoti kubwa kwa timu na kuilinda timu yake. Amekuwa akifanikiwa sana kutokana na kuwa rafiki wa wachezaji. Namtakia kila la heri, afya njema na uzima pia".
Comments
Post a Comment