OLIVIER GIROUD AIPELEKA ARSENAL 18 BORA YA CHAMPIONS LEAGUE … Olympiacos yalala 3-0 kwa vijana wa Wenger, Bayern Munich yaendeleza kichapo
Hatimaye Arsenal imepangua wingu            zito lililokuwa limetanda mbele yao kwenye hatua ya makundi ya            Champions League na kuichabanga Olympiacos 3-0 kwenye mchezo            wa kundi F.
        Ushindi huo umetosha kabisa              kuivusha Arsenal kwenda hatua ya 16 bora ikiwa ni mwaka wa              16 mfululizo kutinga hatua hiyo.
        Shujaa wa Arsenal alikuwa ni              mshambuliaji Olivier Giroud aliyefunga mabao yote matatu              katika dakika ya 29 na 49 huku bao lake la tatu akifunga              dakika ya 67 kupitia mkwaju wa penalti.
        Arsenal              ambao walikubali kichapo cha bao 3-2 kutoka kwa Olympiacos              walipocheza kwenye dimba lao la Emirates, Jumatano hii wakiwa              ugenini kwenye uwanja wa Georgios Karaiskakis jijini Athens,              Ugiriki, wakacharuka na kufanya kile kilichohitajika.
                Ili kusonga mbele kwa tofauti ya              mabao, Arsenal ilitakiwa ishinde kwa zaidi ya bao moja ili              kuipiku Olympiakos.
        Katika mchezo mwingine wa kundi F, Bayern            Munich imeendeleza ubabe kwa kuichapa Dinamo Zagreb 2-0 mabao            yote yakifungwa na Robert Lewandowski katika dakika ya 61 na            64.
        Olympiacos: Roberto 4, Elabdellaoui 5, Da Costa 5,            Siovas 5, Masuaku 5, Kasami 5 (Dominguez 71, 5), Milivojevic            5, Seba 5 (Hernani 77, 5), Fortounis 6.5, Pardo 5 (Finnbogason            86), Ideye 5.
        Arsenal: Cech 7,            Bellerin 6.5, Mertesacker 7.5, Koscielny 7.5, Monreal 7,            Ramsey 7.5, Flamini 7, Walcott 7 (Gibbs 72, 6), Ozil 9,            Campbell 8.5 (Oxlade-Chamberlain 90), Giroud 9.5 (Chambers            90).
        Olivier Giroud amekuwa              shujaa wa  Arsenal kwa kufunga magoli yote matatu dhidi ya               Olympiacos na kutinga hatua ya mtoano
        Olivier Giroud              akishangilia na wenzake
        
Comments
Post a Comment