OFFICIAL: CHELSEA YAMTIMUA MOURINHO


OFFICIAL: CHELSEA YAMTIMUA MOURINHO

Mo 6

Club ya Chelea imemtimua kocha wake Jose Mourinho ikiwa ni mezi saba tu tangu kocha huyo akiongoze kikosi cha The Blues kutwaa ubingwa wa ligi ya England maarufu kama EPL

Mourinho, 52, anakuwa amefukuzwa kwa mara ya pili kwenye klabu ya Chelsea baada ya kurejea klabuni hapo mwaka 2013.

Chelsea ilimaliza pointi nane mbele ya timu iliyokuwa ikifutia nafasi ya pili (Manchester City) msimu uliopita na kushinda ubingwawa ligi lakini tayari imeshapoteza michezo tisa ya ligi kati ya 16 hadi sasa huku ikiwa nafasi ya 16 kwenye msimamo wa ligi pointi moja mbele ya timu ambazo zipo kwenye hatari ya kushuka daraja.

Mechi ya mwisho kwa Mourinho ilikuwa ni Jumatatu iliyomalizika kwa Chelsea kupoteza mchezo huo kwa kufungwa bao 2-1 na Leicester City.

Pep Guardiola, Guus Hiddink, Brendan Rodgers na Junde Ramos wamekuwa wakitajwa kama makocha ambao wanaweza kuchukua nafasi ya Mourinho.

Ameiacha Chelsea pointi moja kutoka mstari wa kushuka daraja huku ikiwa imeachwa pointi 20 na vinara wa ligi hiyo Leicester City, huku kikosi hicho kikiwa hakina matumaini ya kumaliza ligi kikiwa ndani ya top four msimu huu kwa ajili ya kufuzu kushiriki michuano ya Champions League msimu ujao.

Hata hivyo, The Blues wamefanikiwa kupenya kwenye michuano ya Ulaya hatua ya 16 bora ambapo watakutana na mabingwa wa Ufaransa Paris St-Germain mwezi February na March 2016.

Mreno huyo pia ameshinda kombe la FA mwaka 2007 na akifanikiwa kutwaa kombe la ligi mara tatu mwaka 2005, 2007 na 2015.



Comments