HATIMAYE kocha Jose Mourinho amekubali kuwa Chelsea            inaangushwa na kukosekana kwa mshambuliaji mwenye uwezo wa            kupiga mabao.
        Amesema, uwezo wa Diego Costa umeshuka hivyo yupo            tayari kumnunua mshambuliaji wa Atletico Madrid, Antoine            Griezmann katika usajili wa Januari.
        "Kwa kweli hatuna namna ni lazima tufanye usajili wa            washambuliaji wawili au watatu katika mwezi Januari," alisema            Joe Mourinho.
        Kocha huyo alikiri kuwa majeruhi kwa Loic Remy na            Radamel Falcao kunamlazimisha kuwatumia viungo katika nafasi            ya ushambuliaji.
        Chelsea Jumamosi ilipigwa mweleka na timu ya            Bournemouth hivyo kuzidi kusota kwenye nafasi ya 14 ikiwa na            pointi 15.
        Gazeti la The Mirror limefichua kuwa Atletico iko            tayari kumwachia staa wake huyo kama itawekewa mezani paundi            mil. 25 pamoja na mchezaji mmoja.
        Imefichuliwa kuwa kukosa mshambuliaji mwingine na            matokeo kuzidi kuwa mabaya kunamlazimisha Mourinho kumpanga            Costa licha ya kuwa na bifu nae.
        
Comments
Post a Comment