Habari za ndani kutoka kwenye vyombo vya habari vya Uingereza wanasema kwamba makubaliano ya Mourihno kwenda Manchester United tayari yameshafanyika. Habari hii inaunganishwa na interview ya wakala wa Jose Mourihno ambae alisema kwamba mteja wake hatakaa nje ya kazi kwa muda mrefu, ndani ya muda mfupi tutamuona tena amerudi kazini.
Habari zinasema kwamba wakala Jorge Mendes ameshafanya makubaliano kilichobakia hadi sasa hivi ni kwamba wanasubiliwa maboss wa Manchester united Glazers kuamua siku gani ya kumwachisha kazi kocha LVG.
Comments
Post a Comment