Arsenal imefanikiwa kukamata uskani wa Ligi Kuu ya England baada ya kushinda 2-0 dhidi ya Bournemouth huo ukiwa ni mchezo wa mwisho katika mwaka 2015.
Katika mchezo huo uliochezwa Emirates, kwa mara nyingine tena Mesut Ozil akaendelea kuwa shujaa wa Arsenal baada ya kuibuka kuwa nyota wa mchezo huku pia akifunga bao la pili dakika ya 63.
Aliyefungua akaunti ya magoli alikuwa ni beki wa Kibrazil Gabriel aliyeifungia Arsenal bao kwanza kunako dakika ya 27.
Arsenal: Cech 7, Bellerin, 6 Mertesacker, 6 Gabriel, 8 Gibbs 7 (Monreal 82mins 6), Chambers, 7 Ramsey 6.5, Oxlade-Chamberlain, 6.5 (Iwobi 90) Ozil,9 Walcott 6, Giroud 7 (Campbell 81, 6.5)
Bournemouth: (4-1-4-1): Boruc 7, Smith, 6 Francis, 7 Cook, 6.5 Daniels, 5.5, Surman 6, Ritchie, 6.5 Gosling, 7 (O'Kane 6) Arter, 6.5 Pugh 6 (Stanislas HT 6), King 6.5 (Murray 81, 6)
Mesut Ozil akiifungia Arsenal bao la pili dakika ya 63
Ozil akishangilia
Hivi ndiyo Gabriel (kulia) alivyofunga bao lake kwa kichwa
Theo Walcott akiangalia juhudi zake zikishindwa kuzaa bao
Comments
Post a Comment