MCHEZAJI HUYU ANAHUSISHWA NA USAJILI WA MANCHESTER UNITED


MCHEZAJI HUYU ANAHUSISHWA NA USAJILI WA MANCHESTER UNITED

MCHEZAJI Breel Embolo anayekipiga FC Basel ya nchini kwao Uswisi, amepigiwa debe kwamba ndio chaguo kubwa la kocha Louis Van Gaal.

Taarifa iliyotolewa na vyombo vyahabari nchini humo, imeeleza kwamba mchezaji huyo huenda akatua katika timu ya Manchester United katika usajili wa dirisha dogo.

Mkali huyo ameanza kufuatiliwa na timu hiyo ili kuondoa kasoro kwenye safu ya ushambuliaji ya timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu nchini Uingereza.

Hata hivyo, hadi juzi, United imeshindwa kutaja dau ambalo wamelitenga kwa ajili ya kutaka kumsajili mkali huyo.



Comments