MSHAMBULIAJI mahiri na mfungaji bora wa muda wote wa            Real Madrid, Cristiano Ronaldo, amelianzisha kwa kusema yeye            na mastaa kadhaa wanaweza kuondoka Santiago Bernabeu.
        Ronaldo amemwambia rais wa Madrid, Florentino Perez            kuwa hawataweza kuendelea kuvumilia matusi na zomea zomea ya            mashabiki wao.
        Alisema hivi sasa wachezaji hawana amani kwenye dimba            la Bernabeu kwani mashabiki wamekuwa wakitaka ushindi kwa kila            mechi, kinyume na hivyo ni matusi na vitisho kwa wachezaji.
        "Sidhani kama inafaa kwa mashabiki kuwatukana na            kuwatisha wachezaji baada ya kupoteza mchezo mmoja kati ya            mechi 20, ni kitu kisichokubalika," alisema Ronaldo.
        Wachezaji wa Real Madrid walikuwa na wakati mgumu            walipokubali kichapo cha mabao 4-0 kutoka kwa mahasimu wao,            Barcelona.
        Licha ya kuungwa mkono na rais wao, Florentino Perez,            wachezaji na hata kocha wao Rafael Benitez, wanaonekana            kutokuwa na amani moyoni.
        .
        Ronaldo alihitimisha kwa kusema kuwa, inaumiza sana            kuona mashabiki ambao wamekuwa wakiwashangilia kila            wanaposhinda, leo wamegeuka na kuwatukana kwa kupoteza mchezo            mmoja.
        Licha ya malalamiko hayo, Ronaldo ameendelea kuwa mwiba            kwa timu pinzani kwa kupachika mabao na jana usiku alifunga            mara mbili katika mchezo wa La Liga dhidi ya Real Sociedad  katika ushindi wa 3-1.
        
Comments
Post a Comment