Mashujaa Band imefumua safu ya uongozi kwa upande wa wanamuziki na kukifutilia mbali cheo cha rais wa bendi.
Nafasi ya rais wa bendi iliyokuwa ikishikiliwa na mwimbaji 'ghali' wa dansi, Chaz Baba, imeondolewa na badala yake sasa kutakuwa na kiongozi wa bendi.
Chaz Baba sasa anakuwa mwanamuziki wa kawaida huku kiongozi wa muda wa bendi akiwa rapa Ferguson.
Mkurugenzi wa Masoko wa Mashujaa, Maxi Luhanga ameithibitishia Saluti5 juu ya mabadiliko hayo na kusema hiyo ni hatua ya mpito hadi hapo wanamuziki watakapofanya uchaguzi kuchagua uongozi mpya.
Akiongea na Saluti5, Chaz Baba aliyevuliwa urais, akasema amefurahishwa na hatua hiyo na anafurahi kuwa mwanamuziki wa kawaida.
"Uongozi ni mzigo na sijambo baya kupokezana mzigo huo, nimefurahia sana mabadiliko hayo, sina kinyogo," alisema Chaz Baba.
Comments
Post a Comment