Safari ya Manchester United katika kusaka mafanikio kwenye Ligi ya Mabingwa barani Ulaya msimu huu, imefikia kikomo baada ya kufungwa 3-2 na Wolfsburg ya Ujerumani.
Kwa matokeo hayo, United imeshika nafasi ya tatu kundi B baada ya PSV kuinyuka CSKA Moscow 2-1 katika mchezo mwingine wa kundi hilo.
Wolfsburg inayoongoza kundi B, inasonga mbele kwenye 16 bora sambamba na PSV iliyoshika nafasi ya pili.
Ili kusonga mbele, United ilihitaji kushinda mchezo huo, lakini mambo yamekwenda kombo licha ya kuongoza kwa bao la mapema kupitia kwa Anthony Martial kunako dakika ya 10.
Wolfsburg ikaenda mapumziko ikiwa mbele kwa bao 2-1 kufuatia mabao ya Naldo dakika ya 13 na Vieirinha dakika ya 29.
United ikasawazisha dakika ya 82 kwa bao la kujifunga la Joshua Guilavogui lakini Naldo akaifungia Wolfsburg bao la ushindi dakika mbili baadae.
Comments
Post a Comment