Manchester United wamekwenda Ujerumani kukubaliana na Wolfsburg kwenye mchezo wao wa mwisho wa Champions League katika kundi B huku wakijua ni ushindi pekee ndiyo utakaowahakikishia nafasi ya kucheza hatua ya mtoano.
Licha ya kuwafunga wakali hao wa Bundesliga kwenye mchezo wa kwanza Old Trafford, lakini United imekuwa ikisotea kupata magoli ya kutosha chini ya Louis van Gaal.
Wamelazimishwa sare ya bila magoli mara tano katika michezo yao tisa ya mwisho na hali ni ngumu zaidi katika kipindi hiki ambacho mshambuliaji wake Wayne Rooney amebaki nyumbani kutokana na kuwa majeruhi.
Manchester United inashika nafasi ya pili katika kundi B ikiwa na pointi 8 huku Wolfsburg wakiongoza kwa pointi 9 ambapo tishio kubwa kwa United ni PSV yenye pointi 7 ambayo itakabiliana na vibonde CSKA Moscow.
Iwapo United itaambulia sare au kipigo huku PSV ikivuna ushindi, basi moja kwa moja kikosi cha Van Gaal kitakuwa kimeaga mashindano.
Manchester United wanajua ni ushindi tu dhidi ya Wolfsburg ndi0 utakaowahakikishia
Kocha Louis van Gaal akisimamia mazoezi ya timu yake kwenye dimba la Volkswagen Arena
Wayne Rooney amebaki nyumbani kutokana na kuwa majeruhi
Msimamo kundi B unavyoonekana
Mshambuliaji wa United Anthony Martial (kushoto) ana kazi kubwa ya kuchuana na beki wa Wolfsburg Dante (kulia)
Comments
Post a Comment