Winga wa Leicester Riyad Mahrez amekuwa bidhaa adimu baada ya Tottenham nayo kuhusishwa na usajili wa            nyota huyo wa kimataifa wa Algeria.
        Manchester United            imekuwa klabu ya kwanza kuhusishwa na Mahrez ambaye ameifungia  Leicester mabao            14 msimu huu.
        Klabu zote hizo            mbili zinatajwa kuwania saini ya Mahrez katika usajili wa dirisha dogo la            Januari ingawa Leicester            imeshapiga mkwara kuwa haitauza mchezaji yoyote katikati ya            msimu.
        Leicester            inaongoza Premier League kwa pointi 38 na katika hali ya            kawaida, haitarajiwi kuingia kwenye mipango ya kubomoa timu            kwa kuuza nyota wake hali itakayoodhohofisha mbio zao za            kusaka taji la Ligi Kuu.
        Manchester United na              Tottenham wanapigana vikumbo kwa Riyad Mahrez
        Mahrez alifunga goli              lake la 13 na 14  kwa njia ya penalti dhidi ya Everton              Jumamosi iliyopita
        
Comments
Post a Comment