MANCHESTER UNITED NA KIWEWE CHA USAJILI ...SASA WATAJWA KUMWANIA GARETH BALE DIRISHA DOGO LA JANUARI
MANCHESTER United imehusishwa na usajili ulio sawa na njozi za mchana za kumnasa straika wa Real Madrid, Gareth Bale katika dirisha dogo la Januari.
Mchezaji huyo wa zamani wa Tottenham ametajwa katika orodha ya usajili wa kocha wa Maashetani hao, Louis Van Gaal ambaye anapambana kuokoa kibarua chake.
Hata hivyo tayari Real Madrid imekanusha juu ya Bale kuhamia United ambayo katika siku za hivi karibuni imekuwa ikihusishwa na usajili wa wachezaji kadhaa wa kadha.
Mbali Bale, pia United imekuwa ikihusishwa kutaka kumrejesha kikosini straika wake wa zamani, Cristiano Ronaldo.
Hata hivyo, mara kadhaa Ronaldo amekuwa akizungumzia suala la yeye kurejea Old Trafford kuwa ni jambo linalowezekana, ila linahitaji subira ya kipindi kirefu kijacho.
Taarifa za usajili za hivi karibuni zinasema, Bale amekuwa chaguo la kwanza katika orodha ya usajili wa Old Trafford huku ikidaiwa kuwa Van Gaal anahitaji mchango wa mwanandinga huyo aliyetua Madrid kwa dau nono la pauni mil. 80.
Tayari Man United imeweka mezani kitita cha pauni mil. 60 kwa aili ya kumnasa Bale, huku kukiwa na tarifa za kutaka kuongeza dau zaidi.
Comments
Post a Comment