MANCHESTER CITY YAKAMATA USUKANI PREMIER LEAGUE WILFRIED BONY AKIIUA TIMU YAKE YA ZAMANI



MANCHESTER CITY YAKAMATA USUKANI PREMIER LEAGUE WILFRIED BONY AKIIUA TIMU YAKE YA ZAMANI

Wilfried Bony amefunga bao moja dakika ya 26 dhidi ya timu yake ya zamani Swansea City na kuchangia kuipa Manchester City pointi tatu muhimu kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England.

Katika mchezo huo uliochezwa Etihad Stadium, City imevuna kwa mbinde ushindi wa bao 2-1 huku Swansea ikijilaumu yenye kupoteza mechi hiyo baada ya kusawazisha dakika ya 90.

Bafetimbi Gomis aliifungia bao Swansea ambalo lingewafanya waambulie pointi moja, lakini kabla hawajamaliza furaha yao, Yaya Toure akaifungia Manchester City ndani ya dakika tatu za majeruhi.

Ushindi huo umeifanya Manchester City irejee kileleni mwa Ligi Kuu kwa pointi 32 na kuishusha Leicester City kwa tofauti ya magoli.

Leicester City ambayo nayo ina pointi 32 itakuwa na kibarua cha kusaka tena nafasi ya kwanza wakati itakapomenyana na Chelsea Jumatatu usiku.

Arsenal yenye pointi 30 nayo itakuwa na nafasi nzuri ya kuongoza ligi iwapo itainyuka Aston Villa Jumapili jioni.

Matokeo ya mechi zote zilizochezwa Jumamosi jioni ni:
Norwich City 1 - 1 Everton
Crystal Palace 1 - 0 Southampton
Manchester City 2 - 1 Swansea City
Sunderland 0 - 1 Watford
West Ham United 0 - 0 Stoke City






Comments