Manchester United na Chelsea zimetoshana nguvu katika mchezo wa Premier League uliochezwa Old Trafford baada ya timu hizo kutoka sare ya 0-0.
Kama kuna wachezaji waliokuwa mashujaa kwenye mchezo huo, basi walikuwa ni makipa wa timu zote mbili David de Gea na Thibaut Courtois ambao walifanya kazi ya ziada langoni.
Makipa hao ndiyo waliokuwa sababu kubwa ya kufanya mchezo uishe kwa sare ya bila magoli baada ya kuokoa mikwaju kadhaa iliyokuwa ikionekana dhahiri kuelekea nyavuni.
MANCHESTER UNITED (4-2-3-1): De Gea 8.5; Young 7, Smalling 6, Blind 5.5 (Jones 81), Darmian 6 (Borthwick-Jackson 70, 6.5); Schneiderlin 7, Schweinsteiger 6.5; Mata 6 (Depay 77, 5), Herrera 7, Martial 7.5; Rooney 6
CHELSEA (4-2-3-1): Courtois 8; Ivanovic 5, Zouma 6.5, Terry 6.5, Azpilicueta 6; Mikel 6, Matic 5; Willian 5.5 (Ramires 70, 6), Oscar 6, Pedro 6.5; Hazard 7.5
Nemanja Matic alipoteza nafasi ya wazi ya kufunga baada ya kupaisha mpira juu
Nyota huyo wa kimataifa wa Serbia akijilaumu baada ya kushindwa kukwamisha mpira wavuni
Kiungo wa Manchester United Ander Herrera alipoteza nafasi ya kufunga pale kipa cha Chelsea Thibaut Courtois aliporuka na kupangua mpira
Hapa sasa ilikuwa ni zamu ya Herrera kujilaumu
Comments
Post a Comment