Liverpool inazidi kukwea vidato kwenye Ligi Kuu ya            England baada ya kuifunga Sunderland 1-0 katika mchezo            uliochezwa Jumatano usiku.
        Bao pekee la Liverpool lilifungwa na Christian Benteke            sekunde chache baada ya mapumziko.
        Kwa ushindi huo Liverpool sasa imesogea hadi nafasi ya            saba, pointi moja nyuma ya Crystal            Palace iliyoko nafasi ya tano.
        Lakini ushindi huo unaifanya Liverpool            ifungane pointi na  Manchester            United inayoshikilia nafasi ya sita.
        
Comments
Post a Comment