Makocha Jurgen Klopp na Tony Pulis waliingia kwenye mikwaruzo baada ya Liverpool kupata sare ya 2-2 dhidi ya West Brom kwenye uwanja wa Anfield.
Jurgen Klop kocha wa Liverpool alishindwa kuzuia hisia zake pale Divock Origi alipofunga bao la kusawazisha dakika ya 96.
Kocha huyo akashangilia hadi jirani na mpinzani wake. Kilichofuata ni makocha hao kutiana mkononi kabla hawajatenganishwa ambapo Jurgen Klop akaendelea kushangilia mbele ya jukwaa kuu.
Huo ulikuwa mchezo wa Premier League uliochezwa Anifield ulioshuhudia Liverpool wakipata bao la kuongoza dakika ya 21 kuptia kwa Jordan Henderson.
Craig Dawson akaisawazishia West Brom dakika nane baadae kwa shuti la karibu kufuatia makosa ya kipa Simon Mignolet.
Dakika ya 73 Jonas Olsson akaipa West Brom bao la pili, bao lililodumu hadi dakika ya sita ya muda wa majeruhi pale Divock Origi alipoisawazishia Liverpool.
LIVERPOOL (4-2-3-1): Mignolet 4: Clyne 7, Skrtel 6, Lovren 6 (Origi 76mins), Moreno 7: Can 6.5, Henderson 7: Milner 7, Coutinho 6.5 (Ibe 71mins 7), Lallana 7: Benteke 6
WEST BROM (4-5-1): Myhill 7: Dawson 7, McAuley 8, Olsson 8, Evans 7: McLean 7, Gardner 5, Fletcher 7, Morrison 7, Brunt 7: Rondon 6
Mshambuliaji wa Liverpool Divock Origi akishangilia bao lake la kusawazisha katika dakika za majeruhi
Bao la Origi lilimtia wazimu kocha wa Liverpool
Olsson akiifungia West Brom kwa kichwa
Olsson akishangilia na wachezaji wenzake wa West Brom bao lake la dakika ya 73
Henderson, ambaye amecheza ameanza kwa mara ya kwanza tangu mwezi Agust, akiifungia Liverpool goli la kwanza
Henderson akishangilia kwa hisia kali bao lake la dakika ya 21
Henderson akipongezwa na Christian Benteke baada ya kuifungia Liverpool bao la kuongoza
Henderson ambaye kwa msimu wote huu amekuwa akisumbuliwa na majeraha, akiwa ishara ya upendo mashabiki wa Liverpool
Comments
Post a Comment