LIONEL MESSI AICHEZEA BARCELONA MCHEZO WA 500 KWA USHINDI WA KISHINDO ...Suarez hazuiliki, Neymar akosa penalti
Huu ulikuwa ni usiku wa kihistoria Nou Camp kwa sababu kadha wa kadha - lakini moja itakayokumbukwa zaidi ni ya Lionel Mess kuichezea Barcelona mchezo wa 500.
Barcelona pia ikawaonyesha mashabiki wake waliojazana Nou Camp mataji matano waliyotwaa mwaka huu ikiwemo ya Klabu Bingwa ya Dunia kabla hawajafunga magoli yaliyovunja rekodi ya Real Madrid kwa kufikisha magoli 18o kwa mwaka mzima. Real Madrid walikuwa wanashikilia rekodi hiyo kwa magoli 178.
Messi hakukubali kusherehekea mchezo wake wa 500 bila kutikisa nyavu ambapo dakika ya 33 alifunga bao na kuifanya Barcelona iwe mbele kwa magoli 2-0 kufutia lile la kujifunga la Heiko Westermann dakika ya 29.
Heiko Westermann alijifunga katika juhudi za kuokoa mpira sekunde chache baada ya Neymar kukosa penalti iliyogonga mwamba na mpira kurejea uwanjani na ambapo Ivan Rakitic aliukimbilia kabla hajamgonga Westermann na kujaa wavuni.
Luis Suarez naye hakubaki nyuma, akatupia wavuni mabao mawili katika dakika ya 46 na 83 na kuihakikishia ushindi Barcelona yenye kuongoza ligi kwa tofauti ya pointi tatu.
BARCELONA: Bravo 6.5, Alves 7.5, Vermaelen 7, Mascherano 7, Mathieu 6.5 (Adriano 67, 7), Busquets 8.5 (Bartra 57, 6), Rakitic 7, Sergi Roberto 8 (Munir 86), Messi 9, Suarez 9.5, Neymar 9
REAL BETIS: Adan 9, Molinero 7, Bruno 6 (Pezzella 17), Westermann 6.5 (Digard 36), Vargas 7, N'Diaye 5.5, Petros 6, Cejudo 6.5, Dani Ceballos 8, Van Wolfswinkel 6, Ruben Castro 6 (Van der Vaart 75)
Lionel Messi akicheza mchezo wake wa 500 kwa Barcelona Jumatano usiku katika ushindi wa La Liga dhidi ya Real Betis
Barcelona walizawadiwa penalti baada ya kipa Antonio Adan kugongana na Lionel Messi wakati wakiwania mpira
Neymar alikosa penalti lakini Ivan Rakitic (kushoto) akawa mwepesi kuchukua hatua kabla mpira haujamgonga Heiko Westermann na kuwa bao la kujifunga
Supastaa wa Barcelona akikimbia kushangilia bao lake
Suarez anaendelea kung'ara La Liga kwa kutupia mabao nyavuni
Suarez akiifungia Barcelona bao la nne
Barcelona ikipozi na mataji yake matano iliyotwaa mwaka huu - La Liga, Copa del Rey, Champions League, European Super Cup na World Club Cup
Comments
Post a Comment