Waswahili wana misemo yao, lakini hii ya ligi kuu nchini Ufaransa ni balaa. Klabu ya soka ya Monaco iko katika nafasi ya pili ya msimamo wa ligi hiyo ikiwa na points 32 lakini imeachwa kwa points 19 na vinara Paris Saint Germain, huku tofauti kati ya Monaco (nafasi ya pili) na Tolouse ambao wapo katika mstari wa kushuka daraja ni points 15 tu.
Monaco imepoteza michezo mitatu tu msimu huu pamoja na kutoa sare katika michezo nane, huku wakiipa nafasi PSG ambao hawajapoteza hata mchezo mmoja msimu huu huku wakitoa sare tatu, kuongoza ligi kwa tofauti ya points 19 katika raundi hii ya awali ya ligi.
PSG ambao wako chini ya kocha Laurent Blanc wanaongoza ligi huku wakiwa hawajafungwa mechi yeyote msimu huu, na kwamba wana nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa mapema zaidi kutokana na hali ya ushindani hafifu katika ligi hiyo.
Monaco pamoja na kuwa katika nafasi ya pili na points zao 32 wanaweza kushuka daraja kwani tofauti na timu ya pili kutoka mkiani Toulouse ni alama 15 tu ambapo Kama watapoteza mechi tano inaweza kuwaweka katika hatari ya kushuka daraja pamoja na kuwa katika nafasi ya pili katika sikukuu hizi za krismasi na mwaka mpya.
Uongozi wa mapema wa vinara PSG katika ligi hii unaonesha namna league 1 ilivyokosa ushindani na mvuto miaka hii ya karibuni ukilinganisha na ligi nyingine kubwa Kama England ambapo bingwa hujulikana hadi dakika ya mwisho.
Comments
Post a Comment