Leicester imeshindwa kukanyaga mwaka 2016 ikiwa kileleni mwa Premier League baada ya kulazimishwa sare ya 0-0 na Manchester City.
Ilikuwa ni mechi ngumu iliyoshuhudia miamba miwili inayowania taji ikichuana vilivyo huku kipa wa Manchester City Joe Hart akilazimika kuokoa katika namna ya kuvutia shuti la Christian Fuchs kunako dakika ya 77.
Sare ni matokeo yaliyosyahili ingawa kwa Leicester ni kama ushindi kwao kutokana na namna wengi walivyobashiri kuwa mara baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Liverpool wikiendi iliyopita, basi anguko lao limefika.
Matokeo hayo yamekuwa ni mazuri kwa Arsenal ambayo inaendelea kuongoza ligi kwa tofauti ya magoli huku ikiwa imelingana pointi na Leicester inayobakia nafasi ya pili.
LEICESTER CITY: Schmeichel, Simpson, Huth, Morgan, Fuchs, Inler (Ulloa 67), Drinkwater (King 80), Kante, Mahrez, Vardy, Albrighton (De Laet 92)
MANCHESTER CITY: Hart, Sagna, Otamendi, Mangala, Kolarov, Silva (Navas 74), Fernandinho, Toure, Sterling (Iheanacho 88), De Bruyne, Aguero (Bony 64)
Sergio Aguero kama haamini macho yake kuwa shuti lake limetoka nje
Jamie Vardy (kushoto) akiachia shuti kuelekea lango la Manchester City
Marc Albrighton (aliyelala chini) anashuhudia mpira aliopigia ukigonga nyavu za nje
Raheem Sterling (kulia) akiangalia juhudi zake zikizimwa na kipa wa Leicester Kasper Schmeichel
Riyad Mahrez (katikati) akifanyiwa rafu na beki Nicolas Otamendi
Aguero anaamini alistahili kupewa penalti baada ya kuchezewa rafu na Gokhan Inler ndani ya box lakini refari akaipotezea
Comments
Post a Comment