Licha ya kukingiwa kifua na mmiliki wa timu, mashabiki na wachambuzi kibao wa soka, kibarua cha Jose Mourinho si salama.
Chelsea imechukua kichapo cha bao 2-1 kutoka kwa Leicester City kwenye mchezo wa Ligi Kuu uliochezwa Jumatatu usiku, matokeo ambayo yanaishusha Arsenal hadi nafasi ya pili.
Leicester City inayonolewa na kocha wa zamani wa Chelsea, Claudio Ranieri, imedhihirisha kuwa haina mpango wa kuwa msindikizaji bali ni klabu iliyopania kutwaa taji la Premier League.
Mshambuliaji anayewatesa walinda milango, Jamie Vardy aliunganisha krosi ya Riyad Mahrez Leicester bao kwanza dakika ya 34 na kudumu hadi mapumziko.
Dakika ya 48 Riyad Mahrez akapachika bao la pili kwa wenyeji kabla ya Loic Remy hajafungia Chelsea goli la kufutia machozi dakika ya 77.
Leicester City inangoza ligi kwa pointi 35 ikifuatiwa na Arsenal yenye pointi 33, Manchester City ni ya tatu kwa pointi zake 32 wakati Manchester United ikikamata nafasi ya nne kwa pointi 29.
LEICESTER CITY (4-4-1-1): Schmeichel 7, Simpson 6.5, Morgan 7, Huth 7, Fuchs 7, Mahrez 8.5 (Inler 82), Drinkwater 5 (King 17, 6), Kante 8, Albrighton 7, Ulloa 7, Vardy 8 (Okazaki 88).
CHELSEA (4-2-3-1): Courtois 6.5, Ivanovic 6, Zouma 5, Terry 4.5 (Fabregas 53, 5), Azpilicueta 5, Ramires 5, Matic 6, Willian 6, Oscar 6 (Remy 65, 7), Hazard 5 (Pedro 30, 6.5), Costa 5.
Chelsea wakiwa hoi wakati wakizamishwa kwenye mchezo wa Premier League
Jamie Vardy akishangilia bao la kwanza
Jamie Vardy akifunga bao lake la 15 msimu huu baada ya kuwazidi maarifa John Terry na Kurt Zouma
Riyad Mahrez akishangilia bao la pili la Leicester City
Loic Remy akiifungia Chelsea bao pekee huku kipa Kasper Schmeichel akiwa hana la kufanya
Comments
Post a Comment