Mashabiki wameshaanza kumiminika nchini Japan tayari wanazi-count down siku zilizobaki ili kuanza kwa michuano ya FIFA Club World Cup ambapo mabingwa wa mabara sita pamoja na nchi mwenyeji zitakapochuana kuwania taji hilo kubwa kwa upande wa vilabu.
Mchuano wa kufungua dimba utakuwa kati ya Sanfercce Hiroshima dhidi ya Auckland City unakaribia, kuelekea michuano hiyo mtandao huu umepekua kwenye rekodi mbalimbali za michuano hiyo na kuibuka na baadhi ya rekodi ambazo zimewekwa kwenye mashindano hayo (Club World Cup) kwa miaka kadhaa sasa lakini hii ni katika kuhakikisha haupitwi na vitu vizuri.
73,000 namba ya mashabiki ambao walihudhuria kwenye mechi ya ufunguzi hatua ya makundi kati ya Manchester United dhidi ya Vasco da Gama kwenye jiji la Rio de Janeiro mwaka 2000 namba ambayo irijirudia tena kwenye mchezo wa fainali kati ya Corinthians dhidi ya Vasco. Mahudhurio hayo yameweka rekodi kwenye michuano ya Club World Cup.
1.93 Urefu (kwa mitres sawa na futi 6'4) wa beki wa kati wa Barcelona Gerard Pique, beki wa TP Mazembe Salif Coulibaly na golikipa wa Guangzhou Evergande Li Suai ambao ni ndiyo wanasadikiwa kuwa wachezaji warefu zaidi kwenye michuano hiyo mwaka 2015. Kwa upande wa mchezaji mfupi zaidi kwenye michuano hiyo ni mshambuliaji wa TP Mazembe Soloman Asante, yeye ana urefu wa mita 1.59 sawa na futi 5'3.
39. Ni umri wa golikipa wa TP Mazembe Robert Kidiaba, mchezaji mwenye umri mkubwa kwenye mashindano ya mwaka huu wakati kiungo wa Auckland City Clayton Lewis ni mchezaji mdogo kabisa kwenye michuano hiyo.
11.Rekodi ambayo imewekwa na wachezaji watatu wa Misri Wael Gomaa, Hossam Ashour na Mohamed Aboutrika ambao wote wamecheza jumla ya mechi 11 za mashindano hayo wakiwa na Al Ahly.
8. Idadi kubwa ya magoli ambayo yamewahi kufungwa kwenye mchezo mmoja wa Club World Cup. Mchezo huo ulikuwa wa nusu fainali kati ya Manchester United dhidi ya Gamba Osaka ulipigwa Japan mwaka 2008 ambapo Man United ilishinda kwa magoli 5-3.
3. Namba ya wachezaji ambao wamewahi kucheza na kufunga wakiwa kwenye na timu zaidi ya moja kwenye michuano ya Club World Cup. Ronaldinho (Barcelona pamoja na Atletico Mineiro), Dwight Yorke (Manchester United na Sydney FC) pamoja na Neri Cardozo (Boca Juniors na Monterrey) ni wachezaji pekee ambao wamecheza kwenye michuano hiyo wakiwa na timu tofauti zaidi ya moja.
7. Klabu ya Auckland City watakuwa wanacheza michuano hiyo kwa mara ya saba, wakiipiku miamba ya Misri Al Ahly mara mbili zaidi. Michuano iliyopita iliyofanyika Morocco, klabu hiyo ilimaliza nafasi ya tatu kwenye michuano hiyo.
1. Timu ambayo inacheza michuano ya Club World Cup kwa mara ya kwanza 2015. River Plate ndiyo klabu pekee ambayo inacheza michuano hiyo kwa mara yake ya kwanza tofauti na baadhi ya timu ambazo kati ya hizo zinine zilikuwepo kwenye michuano iliyofanyika Morocco mwaka 2014. Timu 54 tayari zimeshawahi kucheza mashandano hayo, River Plate inakuwa timu ya 55 kushiriki michuano hiyo.
5. Magoli yaliyofungwa na mshambuliaji raia wa Argentina Cesar Deldado ambaye ndiye anaongoza kwa kuwa na magoli mengi. Striker huyo aliweka rekodi hiyo baada ya kucheza back-to-back mwaka 2012 na 2013. Lionel Messi ndiyo mshambuliaji anayemfuatia akiwa na mabao manne na huenda akaivunja rekodi hiyo ya Delgado baada ya kumalizika kwa michuano ya mwaka huu.
2.5 Wastani wa magoli ambayo yalifungwa kwenye michuano ya 2014 iliyofanyika Morocco. (magoli 20 ndani ya mechi nane). 3.5 wastani mkubwa wa magoli yaliyowahi kufungwa kwenye historia ya mashindano hayo, rekodi hiyo iliwekwa kwenye michuano ya mwaka 2013.
5. Idadi ya wachezaji ambao wameshawahi kutwaa taji la Club World Cup wakiwa na timu mbili tofauti. Dida (Corinthins mwaka 2000 na AC Milan 2007), Danilo (Sao Paulo mwaka 2005 na Corinthians mwaka 2012, Thiago (Barcelona mwaka 2011 na Bayern Munich mwaka 2013), Cristiano Ronaldo (Manchester United 2008 na Real Madrid mwaka 2014), pamoja na Toni Kroos (Bayern Munich 2013 na Real Madrid mwaka 2014).
Comments
Post a Comment