KUELEKEA ARSENAL VS MAN CITY, HII NI HABARI MPYA KUHUSU AGUERO, SANCHEZ


KUELEKEA ARSENAL VS MAN CITY, HII NI HABARI MPYA KUHUSU AGUERO, SANCHEZ

 aguerosanchez1

Mara baada ya kuwa nje ya uwanja kwa majuma kadhaa hivi sasa mshambuliaji Sergio Kun Aguero wa klabu ya soka ya Manchester City wiki hii amefanya mazoezi na kikosi cha kwanza cha kocha Manuel Pellegrini na kwamba yuko tayari kuikabili Arsenal kwenye mchezo wa leo.

Arsenal na Manchester City zitapambana katika mchezo wa ligi kuu soka nchini England katika uwanja wa nyumbani wa Arsenal, Emirates majira ya saa tano usiku huku timu zote mbili zikiwania ushindi kujaribu kubanana na vinara Leicester City.

Arsenal wanashika nafasi ya pili nyuma ya Leicester yenye points 38 huku Arsenal wakiwa na points 33 wakati City wakiwa na points 32. Hivyo ushindi wowote kati ya timu zote mbili ni muhimu kuikaribia Leicester ambao wanaongoza ligi wakiwa wamepoteza mechi moja tu tangu kuanza kwa msimu.

Sergio Aguero ni mchezaji muhimu katika kikosi cha City, ambapo msimu uliopita alitwaa kiatu cha dhahabu kama mfungaji bora wa ligi. Uwezo wake wa upachikaji mabao unamfanya kuwa moja ya washambuliaji tishio zaidi ulimwenguni.

Arsenal kwa upande wao bado wamekua na wimbi kubwa la majeruhi huku mshambuliaji wao hatari Alexis Sanchez akiwa nusu kwa nusu kucheza mechi ya leo baada ya kuwa majeruhi tangu wiki iliyopita. Wachezaji wengine muhimu ambao ni majeruhi ni pamoja na kiungo mkabaji Coquelin.



Comments