KOCHA LIVERPOOL AJIPA MOYO, ASEMA HAKUNA TIMU INAYOMNYIMA USINGIZI



KOCHA LIVERPOOL AJIPA MOYO, ASEMA HAKUNA TIMU INAYOMNYIMA USINGIZI

Licha ya mwendo wa kusuasua, kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema kwamba amejipanga vyema na kamwe haoni kama kuna timu yoyote inawatisha katika michuano mbalimbali inayowakabili.

Klopp aliyasema hayo wakati akiongea na waandishi wa habari na kudai kuwa amegundua kikosi chake kiko vizuri licha ya kuwepo kwa kasoro kadhaa hasa upande wa ushambuliaji ambapo wamekuwa wanapoteza nafasi nyingi za kupachika mabao.

Alisema, hakuna timu yoyote ambayo inampa presha hivi sasa kwenye michuano ya Ligi Kuu na michuano mingine  kwa vile vijana wake wapo sawasawa licha ya kukabiliana na upinzani mkali.


"Sitishwi na timu yoyote, tupo makini kufanya vema katika michuano inayotukabili," alisema kocha huyo.


Comments