Premier League ya mwaka huu si mchezo, Liverpool imechukua kipigo kitakatifu cha bao 3-0 kutoka kwa Watford na kudhihirisha kuwa kubadilisha kwao kocha bado sio suluhisho la mwendo wao wa kusuasua.
Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp, aliyekuwa akisaka ushindi wake wa kwanza Premier Leguea tangu mwezi Disemba uanze, akajikuta akiishuhudia timu yake ikiwa nyumba kwa bao 2-0 ndani ya dakika 15 za mwanzo.
Katika mchezo huo ambao Liverpool ilishindwa kabisa kufurukuta, Nathan Ake akaifungia Watford bao la kwanza dakika ya 3 ya mchezo huku Odion Ighalo akifunga magoli mawili dakika ya 15 na dakika ya 85.
Watford (4-4-2): Gomes 7; Nyom 6, Britos 7, Cathcart 7, Ake 7; Abdi 7 (Behrami 79), Watson 7, Capoue 8, Jurado 7 (Anya 76); Deeney 7.5, Ighalo 7.5 (Guedioura 88).
Liverpool (4-3-3): Bogdan 4; Clyne 5, Skrtel 4 (Origi 40, 6), Sakho 5, Moreno 5; Henderson 5, Leiva 6, Can 5; Lallana 6 (Ibe 74, 5), Firmino 4 (Benteke 74, 5), Coutinho 4.
Ake (katikati) akishangilia bao lake
Odion Ighalo akisherehekea goli lake
Nyota wa Watford Deeney na Ighalo wakipongezana kwa ushindi
Comments
Post a Comment