Badaa ya mchezo wa African Sports dhidi ya Yanga kumalizika jana kwenye uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, kocha wa magolikipa wa Yanga Juma Pondamali 'Mensa' alimvaa kocha mwenzake wa magolikipa wa timu ya African Sports Razack Siwa akitaka kuzichapa 'kavukavu' kwa madai kwamba kocha huyo amekuwa akitaka kukitia mchanga 'kitumbua' chake.
Pondamali amesema kocha huyo wa makipa wa Sports amekuwa akituma message kwa makocha wa Yanga akidai Pondamali aondolewe kwenye nafasi hiyo ya kuwafundisha magolikipa wa Yanga ili yeye achukue nafasi hiyo kwasababu anauzoefu kuliko Pondamali.
Mensa amesema, alimvaa Siwa ili amwambie ukweli kuhusu kuacha mpango wake wa kuwatumia ujumbe makocha wa Yanga kuwaomba wamtimue ili yeye aingie kufundisha magolikipa wa Jangwani.
"Analeta ujinga mmoja kwasababu yeye alikuwepo hapa sasa tangu kipindi Maximo yupo alikuwa anamtumia message zaidi ya mara tatu kwamba aniondoe mimi amrudishe yeye. Mimi jana nikamfata nikamwambia utarabu huu unaoufanya haupo kwenye kazi, yeye asubiri mimi nitaondoka halafu yeye utakuja kuomba kazi", alisema Mensa kwa jazba.
"Kaja kocha huyu katafuta namba yake ameipata, sasa tulikuwa mazoezini na mwalimu akanionesha message kwamba yeye anataka kuja yeye ni mzoefu kuliko mimi. Baada ya mechi ya jana mimi nikamfata nimwambie ukweli".
Siwa amethibitisha sakata hilo kutokea jana huku akisema ni amekua akiomba nafasi ya ukocha wa magolikipa kwenye kikosi cha Yanga.
Comments
Post a Comment