Jose Mourinho yupo tayari, tena mwenye utashi kupita maelezo ya kumrithi Louis van Gaal iwapo kocha huyo wa Uholanzi atatimuliwa Manchester United.
Kibarua Van Gaal kiko hatarini baada ya mwendo mbovu uliopekelea Manchester United kushinda mechi tatu tu katika michezo yake 13 ya mwisho katika mashindano yote.
Jose Mourinho alitimuliwa Chelsea katikati ya wiki iliyopita na sasa nafasi iko wazi kwake kujiunga na Manchester United iwapo Van Gaal atafungasha virago.
Licha ya bodi ya Manchester United kumpa kura ya imani Van Gaal huko nyuma, lakini kipigo cha 2-1 kutoka kwa Norwich Jumamosi iliyopita kwenye mchezo wa Ligi Kuu, kimeamsha wasiwasi wa maisha ya kocha huyo Old Trafford.
Van Gaal mwenyewe amekiri kuwa sasa anaanza kuhofia kibarua chake Manchester United na kukiri kuwa iwapo timu haitaanza kushinda basi atakuwa hayuko salama.
Jose Mourinho (katikati kushoto) yupo tayari kumrithi Van Gaal iwapo atatimuliwa
Mourinho huenda akamrithi Van Gaal
Van Gaal hati hati Manchester United
Comments
Post a Comment