KOCHA wa Chelsea, Jose Mourinho amesema kuwa            mshambuliaji wa Leicester City, Jamie Vardy (pichani kulia)            ana ubora wa kucheza klabu yoyote duniani.
        Mshambuliaji huyo kwa sasa anaongoza kwa upachikaji            mabao katika michuano ya Ligi Kuu England, ambapo hadi sasa            ana jumla ya mabao 14 huku akifuatiwa na mshambuliaji wa            Everton, Lumelu Lukaku mwenye mabao 12.
        Kutokana na uwezo wa Vardy, Mourinho anaamini kuwa            mchezaji huyo anaweza kupata mafanikio katika klabu yoyote.
        "Kwa sasa yeye ni mchezaji ambaye anaongoza kwa kufunga            mabao, ninaamini hakuna klabu abayo haimkubali mchezai huyo. 
        "Kutokana na uwezo wake, ninaamini anaweza kucheza            klabu yoyote duniani na kupata mafanikio makubwa kama ilivyo            kwa nyota wengine," alisema Mourinho.
        Vardy mwenye umri wa miaka 28 alivunja rekodi ya            kupachika mabao 11 katika michezo 11 ya mwanzoni mwa michuano            ya Ligi Kuu nchini England hivyo Mourinho anaamini msimu ujao            hakuna mchezaji ambaye anaweza kuvunja rekodi ya mchezaji            huyo.
        "Ameweka rekodi ya aina yake, sina hakika kama kuna            mchezaji ambaye anaweza kupachika mabao 11 katika michezo ya            mwanzoni na kuvunja rekodi yake, itakuwa ni ndoto," alisema            Mourinho.
        
Comments
Post a Comment