Kipa wa Manchester City Joe Hart amesisitiza kuwa timu yao ilistahili kuwa kileleni mwa Premier League katika kipindi hiki ambacho ligi imefikia katikati ya msimu.
Kikosi cha Manuel Pellegrini kinashika nafasi ya tatu kikiwa nyuma kwa pointi tatu dhidi ya vinara Arsenal na hiyo ni baada ya kuambulia sare ya 0-0 kwa Leicester inayoshika nafasi ya pili.
Golikipa huyo namba moja wa England alifanikiwa kulinda vema lango lake kutoka kwa wafungaji wenye uchu Riyad Mahrez na Jamie Vardy, lakini anaamini City ilistahili kuondoka na pointi tatu King Power Stadium kutokana na nafasi walizozitengeneza.
Joe Hart anasema Manchester City ilistahili kuongoza ligi
"Hatupo sehemu tunayostahili, hii ni kutokana na kutocheza vema katika baadhi ya michezo yetu," Hart aliiambia tovuti ya Manchester City.
"Tulianza msimu kwa nguvu lakini hatukucheza vizuri katika mechi 12 za mwisho ila tuko kwenye nafasi nzuri na timu zote mbili zilizoko juu yetu zimestahili kuwa hapo.
"Bila shaka yoyote, ili tuwe juu tunalazimika kushinda - kushinda mechi zote za nyumbani na kukomaa ili kushinda pia michezo ya ugenini"
Joe Hart akipangua shuti la Riyad Mahrez (kulia)
Comments
Post a Comment