Wakongwe Steven Gerrard wa Liverpool na Rio Ferdinand wa Manchester United wamewamwagia sifa wachezaji Aaron Ramsey na Laurent Koscienly wa Arsenal kutokana na kuwa katika kiwango cha huu hivi sasa na hata kuisaidia klabu yao kuifunga magoli 3-0 klabu ya Olympiakos Pireus nyumbani kwao na kufanikiwa kusonga mbele katika raundi ya 16 bora.
Wakiongea mara baada ya kumalizika mchezo huo wa Arsenal dhidi ya Olympiakos Pireus, wakongwe hao ambao ni wachambuzi wa mpira hivi sasa katika kituo cha televisheni cha BT Sports, wamesema wachezaji hao ni bora zaidi katika nafasi zao si tu katika klabu yao bali katika ligi kuu nchini England.
Nahodha wa zamani wa Liverpool Steven Gerrard akimzungumzia kiungo Aaron Ramsey amesema, Ramsey ni miongoni mwa viungo bora zaidi wa ushambuliaji katika ligi kuu nchini England. Gerrard amesema kuwa Ramsey amekua hafurahii kucheza nafasi ya kiungo wa kulia, huku akisema kuwa Ramsey ana uwezo mkubwa sana katikati ya kiwanja.
Aidha, Rio Ferdinand akimzungumzia mlinzi Laurent Koscienly amesema kuwa mlinzi huyo akiwa kwenye fomu ni bora kuliko yeyote katika ligi kuu soka nchini England. Rio anasema beki huyo amekua kiongozi wa ulinzi imara na Rio anaamini kuwa kama akiwa katika fomu basi Arsenal inakua bora pia.
Comments
Post a Comment