HOFU YATANDA WACHEZAJI MAN UTD, NI KUHUSU ‘NOTE BOOK’ YA VAN GAAL


HOFU YATANDA WACHEZAJI MAN UTD, NI KUHUSU 'NOTE BOOK' YA VAN GAAL

Van Gaal 3

Gazeti la daily mail la nchini England limeripoti kuwa wachezaji wa klabu ya Manchester United hata kabla ya mchezo wa juzi wa klabu bingwa Ulaya wamekua wakikabiriwa na hofu kubwa kuhofia kuingia katika kitabu cha kocha wao Louis Van Gaal.

Habari zinasema kuwa kocha Louis Van Gaal huandika kola kosa linalofanywa na wachezaji wake wakati wa mechi na mazoezi ya timu hiyo, jambo ambalo linawafanya wachezaji wasijiamini kuhofia kuandikwa katika kitabu hicho ambacho kimejaa makosa ya wachezaji hao.

Man U

Mapema mwezi September mwaka huu, nahodha Wayne Rooney na Michael Carrick walifika ofisini kwa kocha wao na kumuonya kuhusu utaratibu wake wa udhibiti wa wachezaji kwamba sio wa afya kutokana na ukweli kwamba kocha huyo huwabana wachezaji kila sekunde, vikao mara kwa mara, ratiba za chakula na video za makosa ya wachezaji.

Inaelezwa kuwa utaratibu huo huwakera na kuwachosha wachezaji ambao hukosa kujiamini. Angel Di maria anatajwa kuwa miongoni mwa sababu zilizomuondoa klabuni hapo ni udikteta wa kocha Louis Van Gaal, huku Memphis Depay nae akionywa.

Matatizo haya ya kocha Louis Van Gaal yameigharimu klabu hiyo na sasa wametolewa nje ya michuano ya klabu bingwa Ulaya katika hatua ya makundi huku wakiwa hali ya kuchechemea katika ligi kuu soka nchini England.



Comments