HATIMAYE JOSE MOURIHNO AFUNGUKA: "NINASALITIWA NA WACHEZAJI CHELSEA"


HATIMAYE JOSE MOURIHNO AFUNGUKA: "NINASALITIWA NA WACHEZAJI CHELSEA"
Mourinho, fighting for his job                with Chelsea in unprecedented waters, said. 'I feel my                work was betrayed'
Hatimaye kocha wa Chelsea Jose Mourinho amewashutumu baadhi ya wachezaji wake na kusema wanamsaliti kufuatia kipigo cha 2-1 kutoka kwa Leicester City katika mchezo wa Premier League uliofanyika Jumatatu usiku. 

Kocha huyo amehoji iwapo kweli wachezaji wake wanaonyesha uwajibikaji wa kweli baada ya kipigo cha tisa msimu huu na kubakia pointi moja tu juu ya janga la kushuka daraja.

Aidha, Mourinho pia amehoji uwajibikaji wa  Eden Hazard baada ya nyota huyo wa kimataifa wa Ubelgiji kujiondoa mwenyewe dimbani kwa madai ya kuumia paja kipindi cha kwanza.

Leicester walicheza soka bab kubwa na kurejea kileleni mwa Ligi Kuu kupitia magoli ya Jamie Vardy na Riyad Mahrez ambao kwa pamoja wana jumla ya magoli 26 katika Premier League msimu huu. 

Licha ya Loic Remy kuifungia Chelsea bao pekee dakika ya 77, lakini bado timu hiyo haikuonyesha mapambano ya dhati ya kusaka pointi katika kipindi hiki ambacho Mourinho anapigania kibarua chake kwa kila hali.

"Ninahisi kazi yangu inasalitiwa," alisema Mourinho. "Tuliruhusu magoli mawili katika namna ambayo kwangu inanipa mashaka.

"Najua kuwa moja ya ubora wangu ni namna ya kuusoma mchezo kwa wachezaji wangu, kusoma wapinzani na kubaini tishio kutoka kwa wapinzani wetu. 

"Vardy alikwenda katikati ya mabeki wawili wa kati na kufunga bao la kwanza, Mahrez  akawa na mtu mmoja kwenye box lakini mimi nataka watu wawili. Nahitaji mchezaji wa kiungo akabe ipasavyo. Aina ya magoli mawili tuliyofungwa ni jambo gumu kulipokea.

"Mechi hii niliifanyia kazi kwa siku nne. Nilifundisha kila kitu kuhusiana na wapinzani wetu. Nikataja nyendo zao nne za hatari ambazo ndizo walizotumia kwa kiasi kikubwa kufunga kila bao dhidi yetu.

"Wachezaji wangu walipata maelekezo yote mazoezini ndani ya siku tatu za mwisho. Unaweza kuwauliza wao. Najua ni waungwana na watakuambia ninachosema ni ukweli mtupu."
Chelsea manager Jose Mourinho reacts during a ninth                  Premier League defeat of the season at Leicester
Kocha wa Chelsea  Jose Mourinho akishangaa kwenye mchezo wa Premier League dhidi ya Leicester
Jamie                  Vardy celebrates after scoring the opening goal of the                  Premier League game against Chelsea 
Jamie Vardy anashangilia bao lake dhidi ya Chelsea


Comments