Akihojiwa na radio moja nchini Hispania mshambuliaji wa klabu ya soka ya Chelsea Diego Costa amesema siku zote moyo wake uko Atletico Madrid huku akisema anaweza kurudi kuichezea klabu hii siku moja na kuwafuata marafiki zake wa siku nyingi akiwamo mlinzi wa kushoto Fillipe Luiz.
Mshambuliaji huyo hana msimu mzuri hivi sasa Chelsea, amekua akigombana na kocha wake Jose Mourinho hivi karibuni huku akishuhudia kuwekwa benchi mara kwa mara hivi karibuni kutokana na kutokua na kiwango kile cha msimu uliopita.
Costa anasema hufuatilia siku hadi siku klabu yake ya zamani Atletico Madrid ambayo ndiyo iliyomtambulisha kwa kiwango kikubwa. Anasisitiza mapenzi yake yake kwa klabu hiyo na kwamba anaweza kurejea kuchezea hapo na kujumuika na kocha Diego Simeone.
Taarifa zinasema klabu ya Chelsea inajiandaa kunasa saini za wachezaji Antoine Griezman wa Atletico Madrid, mshambuliaji Philipe Anderson wa Lazio katika kutaka kutatua tatizo la ufungaji katika kikosi chao huku pia kutaka kuziba pengo la mshambuliaji huyo endapo ataondoka.
Comments
Post a Comment