DE GEA NAE KAIBUKA NA STORY KUHUSU VAN GAAL



DE GEA NAE KAIBUKA NA STORY KUHUSU VAN GAAL

De Gea 7

Golikipa wa Manchester United David De Gea amezitupilia mbali tuhuma za kwamba wachezaji wa kikosi cha 'mashetani wekundu' hawana furaha chini ya kocha Lois van Gaal kutokana na style yake ya soka. Ripoti za hivi karibuni zimekuwa zikidai kuwa wachezaji wakongwe hawakubaliani na kocha huyo kwenye vyumba vya kubadilishia nguo lakini mkali huyo wa Hispania amesema kila kitu kiko sawa.

"Kwenye vyumba vya kubadilishia kila kitu kiko shwari na kuna umoja, kuna umoja na sote kwa pamoja kama wacheaji tunafuraha na nafikiri hicho ni kitu muhimu kwenye timu kama tunataka kufanikiwa kwenye mambo makubwa", amesema De Gea.

De Gea 8

"Tuna kikosi chenye vijana nafikiri wanakuja vizuri kupitia kwa wakongwe na wanapambana kweli"

"Wachezaji wote ni wazuri na wote wanaiwakilisha Manchester United na naamini taratibu watakuwa wachezaji bora wa baadae na sote tunaamini tuko pamoja".

"Tunafahamu siku zote mwezi December ni mgumu ukiwa na ratiba ya mechi nyingi, na pia wachezaji wanakuwa wamechoka kwahiyo mwisho wa siku tunatakiwa kupata matokeo mazuri. Kwasasa tunalifanyia kazi hilo"

De Gea 9

"Tunajifua kwa nguvu kujiandaa na mechi hizo ili tuwe katika kiwango kizuri ili tupite mwezi December tukiwa kwenye nafasi nzuri karibu na kileleni mwa ligi".

Mashabiki wana hasira timu pamoja na manager baada ya matokeo mabaya ya kuishuhudia United ikitupwa nje ya michuano ya Champions League na Wolfsburg halafu timu ikapoteza tena dhidi ya Bournemouth kwenye mchezo wa ligi weekend iliyopita.

De Gea 10

Inaelezwa baadhidi ya mashabiki wamepanga kupeperusha kipeperushi kinachosema 'Van Gaal' out kwenye mchezo wa weekend hii Manchester United itakapoumana na Norwich City kwenye uwanja wa Old Trafrord.



Comments