Hatimaye kocha wa            zamani wa Everton na Manchester United, David Moyes ametoa            mtazamo wake kuhusu kocha wa sasa wa  United Louis van Gaal.
        David Moyes amesema            Van Gaal anastahili kupewa muda zaidi huku akiamini kuwa            Manchester United inaweza kuzoa mafanikio chini ya Mdachi            huyo.
        Mashabiki wa United            tayari wamepoteza imani kwa Van Gaal huku wakishuhudia klabu            yao iliyokosa soka la kuburudisha ikifunga magoli 13 tu msimu            huu kwenye Premier League.
        Lakini licha ya            shutuma za mashabiki na wachambuzi wa soka, Moyes amedai            mbadala wake huyo anapitia matatizo yale yale aliyopitia yeye            katika uongozi wake wa miezi kumi.
        "Baada ya Sir Alex            kustaafu, kazi ikawa ni ngumu mno," anaeleza Moyes. "Ilihitaji            muda kuijenda upya timu, ilikuwa ni kazi ya kuijenga             Manchester United. Unapaswa pia kukumbuka kuwa David Gill            ambaye alikuwa mhimili mkubwa wa timu naye pia aliondoka.
        "Nadhani hata            utamaduni wa Manchester United uko hivyo, kuwapa muda na            kuwasapoti makocha wake. Nina imani watafanya hivyo kwa Van            Gaal, anastahili kupewa muda zaidi.
        "Bado kuna kazi            anayoitengeneza, amefanya usajili ambao nao unahitaji muda            kabla haujazaa matunda. Kwa uzoefu nilioupata Hispania            inachukua muda wachezaji wa nje kuzoea mazingira mapya."
        David Moyes amemtetea              kocha wa Manchester United  Louis van Gaal
        Van Gaal hajaipa              ushindi United tangu alipoifunga Watford  Novemba 21
          
Comments
Post a Comment