CLAUDIO RANIERI AJIBU MASWALI KUHUSU LEICESTER CITY KUTWAA UBINGWA WA EPL



CLAUDIO RANIERI AJIBU MASWALI KUHUSU LEICESTER CITY KUTWAA UBINGWA WA EPL

Claudio Raniel

Kocha wa Leicester City Claudio Ranieri amesema kwamba atajipa matumaini ya kuchukua 'ndoo' ya Ligi Kuu England endapo ataendelea kubaki kileleni mpaka mwishoni mwa mwezi Aprili.

Leicester City wanatarajiwa kuwa kileleni mpaka siku ya Christmas huku wakiwa na pointi tano juu ya Arsenal ambao ndio wanaowafuatia kwa karibu ambao watacheza na Manchester City kesho.

Ranieri, amesema bado lengo lake kuu ni kufikisha pointi 40 japo kwa sasa ana pointi 38 huku akisema kuwa nafasi waliyopo kwa sasa sio halisi, kwani bingwa hutabiriwa mara baada tu ya kufikisha michezo 36.

Alipoulizwa anajisikije kuwa juu mpaka wakati wa Christmas, alijibu: "Hakuna kitu. isipokuwa inamaanisha tupo katika kiwango bora na tunapata matokeo mazuri.

"Mimi ni mkweli sana. Endapo [kwa nafasi yetu] tuliyopo leo, tutaendelea kuwepo mpaka mwishoni mwa mwezi Aprili basi nitaanza rasmi kufukiria kuhusu ubingwa".

"Kama kunakuwa na michezo miwili imebaki basi hapo nitaanza kufukiria kuhusu ubingwa, lakini kwa sasa hapana!".



Comments