Chelsea imeshinda 3-1 dhidi ya Sunderland katika mchezo wa Ligi Kuu lakini hiyo haikutosha kuwafanya mashabiki wa klabu hiyo wasimkumbuke kocha aliyetimuliwa Jose Mourinho.
Waliimba jina la Mourinho na hata pale majina ya Cesc Fabregas na Diego Costa yalipotajwa uwanjani, mashabiki hao wakazomea kwa nguvu.
Wakati wachezaji hao wakipumzishwa na kwenda benchi huku nafasi zao zikichukuliwa na wachezaji wengine, mashabiki hao wakaimba tena jina la Mourinho kwa nguvu kuonyesha kumuunga kwao mkono.
Mourinho alitimuliwa majuzi baada ya mwendo mbaya msimu huu, lakini mashabiki wa klabu hiyo wamekuwa wakiamini kuwa Mreno huyo amesalitiwa na wachezaji wake ambapo Diego Costa na Fabregas wamekuwa wakihusishwa kwa nguvu na tuhuma hizo.
Magoli ya Chelsea yalifungwa na Branislav Ivanovic, Pedro na Oscar kabla ya Borini hajaifungia Sunderland bao pekee katika dakika ya 53.
Chelsea XI (4-2-3-1): Courtois 6; Ivanovic 7, Zouma 7, Terry 6.5, Azpilicueta 7; Fabregas 7 (Mikel 71 6), Matic 7; Willian 7.5, Oscar 8.5 (Ramires 82 6), Pedro 8; Costa 5 (Remy 75 6)
Sunderland XI (3-4-1-2): Pantilimon 5; Coates 4 (Johnson 23 6.5), O'Shea 5, Kaboul 5.5; Jones 5, M'Vila 6.5, Rodwell 6, Van Aanholt 6; Toivonen 6 (Borini 46 7); Watmore 6 (Graham 79 6), Defoe 6
Branislav Ivanovic (kushoto) akiruka juu kuifungia Chelsea bao la kuongoza
Chelsea wakipata bao la pili kupitia kwa Perdo
Wachezaji wa Chelsea wakiwa wamemzunguka Pedro kumpongeza kwa bao lake
Oscar akiifungia Chelsea bao la tatu kwa mkwaju wa penalti
Mshambuliaji wa Sunderland Fabio Borini akishangilia baada kuifungia timu yake bao pekee dakika ya 53
Atakayekuwa kocha wa muda wa Chelsea Guus Hiddink (kushoto) akiwa na Didier Drogba (katikati) pamoja na tajiri wa timu Roman Abramovich wakifuatialia mchezo dhidi ya Sunderland kwenye uwanja wa Stamford Bridge
Mashabiki wa Chelsea wakionyesha mabango yanayomsapoti kocha aliyetimuliwa Jose Mourinho
Hili ni bango lingine ambalo linamsapoti Mourinho huku likiwashutumu wachezaji na kuwafananisha na Yuda
Bango lenye picha ya Mourinho na maneno yanayosema "Ni mmoja wetu"
Comments
Post a Comment