CHELSEA MOTO CHINI CHAMPIONS LEAGUE, YAILAMBA PORTO 2-0 ...Dynamo Kyiv yainyoa Maccabi Tel Aviv 1 - 0



CHELSEA MOTO CHINI CHAMPIONS LEAGUE, YAILAMBA PORTO 2-0 ...Dynamo Kyiv yainyoa Maccabi Tel Aviv 1 - 0
Baada ya matokeo kadhaa mabaya yaliyotishia uhai wa kibarua cha Jose Mourinho, hatimaye upepo umegeuka na angalau kwa sasa kocha huyo yuko salama salmin baada ya kuivusha Chelsea kwenda hatua ya mtoano ya Champions League (16 bora).

Tajiri wa Chelsea Roman Abramovich, akiwa amekaa na mkewe Dasha Khukova kwenye uwanja wa Stamford Bridge, alishuhudia Chelsea ikiibuka na ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Porto.

Ushindi huo dhidi ya Porto katika mchezo wa kundi G, ni kinga tosha kwa Mourinho lakini shukran zaidi kwake ziwandee Diego Costa na Willian. 

Diego Costa alisababisha goli la kwanza dakika ya 12 baada ya mpira wake uliookolewa na kipa Iker Casillas kumgonga Ivan Marcano na kujaa wavuni huku Willian akitupia bao la pili dakika ya 52.

Chelsea imeshika nafasi ya kwanza kundi G huku Dynamo Kyiv iliyoinyoa Maccabi Tel Aviv 1 - 0 ikikamata nafasi ya pili wakati Porto iliyokuwa ikiongoza kundi hilo kwa muda mrefu ikiangukia nafasi ya tatu na sasa itakwenda kucheza Europa League.

Chelsea (4-2-3-1): Courtois; Ivanovic, Zouma, Terry, Azpilicueta; Ramires, Matic; Willian, Oscar (Pedro 80), Hazard (Remy 89); Diego Costa (Mikel 85)

Porto (4-3-3): Casillas; Maxi Pereira (Neves 57), Marcano Sierra, Maicon, Indi; Herrera (Tello 70), Danilo, Imbula (Aboubakar 56); Corona, Brahimi, Layun 
Willian leaps into the air                  after his second half strike sent Chelsea 2-0 up against                  Porto in the vital Champions League group stage contestWillian akiruka juu kushangilia bao lake
Chelsea striker Diego Costa                  (right) is congratulated by team-mates after his break                  forward led to the opening goal at Stamford Bridge
 Diego Costa (akipongezwa) baada ya juhudi zake kusababisha goli la kwanza
The Spaniard's shot was                  saved by countryman Iker Casillas (right) before                  cannoning off Porto defender Ivan Marcano after 12                  minutesCosta akijaribu kumtungua kipa Iker Casillas (kulia) kabla beki Ivan Marcano hajajifunga dakika ya 12
Maicon's clearance was                  clearly over the goal line and the lead was eventually                  confirmed for Jose Mourinho's side in the 12th minute 
Maicon akijaribu kuoa bila mafanikio
Willian akifunga dakika ya 52
The Chelsea players launch                  onto Willian having moved 2-0 up against Porto to                  confirm the Blues' place in the knockout stages
Wachezaji wa Chelsea wakimrukia Willian kwa furaha
Chelsea owner Roman                    Abramovich (left) smiles and applauds after the                    victory sent Chelsea into the Champions League last                    16
Tajiri wa Chelsea Roman Abramovich (kushoto) akifurahi na mkewe baada ya timu yake kutinga hatua ya mtoano


Comments