NYOTA wa Stoke City, Bojan Krkic amegeuka lulu baada ya vilabu vikubwa barani Ulaya kupigana vikumbo kusaka saini yake.
Miongoni mwa vilabu vinavyotajwa kumwania mchezaji huyo wa zamani wa Barcelona ni pamoja na Manchester United na Chelsea.
Hatua hiyo imekuja baada ya Krkic kung'ara vilivyo msimu huu ikiwa ni pamoja na kuifungia Stoke mabao muhimu likiwemo lile la ushindi wa 2-0 dhidi ya Manchester United Jumamosi iliyopita.
Bojan Krkic akipongezwa na wenzake baada ya kuinyuka Manchester United
Bojan Krkic akifunga dhidi ya Manchester United
Comments
Post a Comment