BAYERN MUNICH YAMPA MKONO WA KWA HERI PEP GUARDIOLA, YAMSAINISHA MIAKA MITATU CARLO ANCELOTTI ...Man City sasa ishindwe yenyewe
Mtendaji mkuu wa Bayern Munich Karl-Heinz Rummenigge amethibitisha kuwa kocha Pep Guardiola anaondoka mwishoni mwa mismu huu na nafasi yake itazibwa na Carlo Ancelotti.
Habari hizo ni njema kwa Manchester City ambao wanatajwa kuwa mbioni kumnyakua Pep Guardiola mwenye umri wa miaka 44.
Guardiola, ambaye ameshinda taji la Bundesliga mara mbili mfululizo tangu alipotua Allianz Arena, amemua kwenda kusaka changamoto mpya pindi msimu huu utakapokamilika huku klabu yake ikiwa kwenye nafasi nzuri ya kutetea taji lake kwa mwaka wa tatu mfululizo.
Carlo Ancelotti ambaye amesaini mkataba wa miaka mitatu ya kuikochi Bayern Munich, hakuwa na timu yoyote tangu alipotemwa na Real Madrid wiki chache kabla msimu huu haujaanza.
Pep Guardiola anaondoka Bayern
Guardiola akiwa mzigoni
Carlo Ancelotti (akikumbatiana na Guardiola in 2014) atakuwa kocha wa Bayern msimu ujao
Bayern Munich imetupia habari ya kuthibitisha kuwa Guardiola ataondoka mwishoni mwa msimu huu
Ancelotti amesaini mkataba wa miaka mitatu kuifundisha Bayern Munich
Ancelotti ameweka kwenye ukurasa wake wa Twitter picha yake iliyoandamana na maneno yanaoonyesha kuwa ni heshima kubwa kwake kupata nafasi ya kuifunisha Bayern Munich
Comments
Post a Comment