Atletico Madrid imeichapa Benfica 2-1 na kushika namba moja kwenye kundi C la Champions League.
Licha ya kipigo hicho, Benfica nayo inasonga mbele kuelekea hatua ya mtoano baada ya kushika nafasi ya pili huku Galatasaray na FC Astana zilizotoka sare ya 1-1 zikiaga michuano hiyo mikubwa barani Ulaya kwa ngazi za klabu.
Comments
Post a Comment