KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger              amekiri kuwa yuko sokoni akisaka nyota wapya katika dirisha              dogo la usajili huku akidai kwamba anahitaji kufanya mageuzi              katika kikosi chake.
        Alisema lengo lake ni kuhakikisha              timu yake inaimarika zaidi na kulinda matokeo mazuri              waliyoyavuna katika nusu ya kwanza ya msimu huku wakiwa              kileleni mwa Premier League.
        "Nataka kubadili mfumo wa              washambuliaji wangu wasipoteze nafasi za kupachika mabao,              tumekuwa tukipoteza nafasi nyingi," alisema Wenger
        Wakati Arsenal ikiaminika kuwa tayari imemnasa kiungo Mohamed Elneny wa Basle,            klabu hiyo pia inahusishwa na usajili wa winga wa  Leicester City, Riyad Mahrez.
        Kiungo mkabaji  wa Basle             Mohamed Elneny anatarajiwa kutua Arsenal kwa pauni milioni            7.4 katika usajili wa Januari
        
Comments
Post a Comment